Rais wa Nigeria amepigwa picha akiwa mjini London kwa mara ya kwanza tangu andoke nchini mwake karibu siku 80 zilizopita.
Rais Muhammadu Buhari mwenye umri wa miaka 74 alisafiri kwenda nchini Uingereza kupata matibabu ya ugonjwa ambao haujulikani.
Siku ya Jumapili alikutana na magavana wa chama chake ambapo alionekena kuwa ni mwenye furaha. kwa mujibu wa taarifa ya serikali.
Kutokuwepo kwake kumezua wasi wasi nchini Nigeria huku wengi wakidai kuwa huenda amefariki.
Wengine wana hofu kuwa huenda asiwe na uwezo wa kurudi kazini.
Bwana Buhari aliondoka Nigeria tarehe 7 mwezi Mei wakati wa safari yake ya pili nchini Uingereza kupata matibabu.
Akiwa hayupo Nigeria, amemuachia madaraka yote makamu wa Rais Yemi Osinbajo
No comments:
Post a Comment