Asalaam akeykum warahmatullah wabarakatu.na pia niwasalim na ndugu zangu katika Adam kwa kusema Tumsifu yesu kristo
Leo tutaangalia nafasi ya Asali katika afya ya nyuso zetu na urembo kwa ujumla wakeASALI ni chakula kitam kitokanacho na nyuki kwa kutumia nekta au maji yenye sukari yatokanayo na maua.
KUNA NIN NDANI YA ASALI?
Katika asali kuana aina kadhaa ya madini magnesium,Potasian,CalciumChumvi aina yaklorini (Sodium chlorine)Salfa Chuma na fosfet
ZAIDI YA HAPO?
Virutubisho vya nyongeza katika asali ni vitamin. B1,B2, C, B6,B5 na B3 ambavyo hubadilika wingi wake kutegamea ubora wa NEKTA
ASALI KATIKA UREMBO WA SURA
Wakina Dada wengi wameamua kuachana na vitu vya asili katika masuala mazima ya urembo wamekuwa wakikimbilia vipodozi ambavyo ndani yake kumekuwa na kemikali nyingi sana na wakina dada hao wakajikuta wanapoteza kabisa uzuri Wa sura zao wengine huungua, kubakiwa na mabaka,wengine hushindwa kutembea juani kwasababu huumia macho na ngozi zao pia kwasababu teyar wanakuwa wameshaatibu kinga zao za ngozi
Maranyingi matabibu hukemea hali hiyo hata mashekh na viongoz mbambali wa kidini hukemea Mimi nakwambia tumia njia wewe unayetaka kutunza ngozi yako .
Chukua asali changanya na limao,ute mweupe wa yai koroga na maziwa ya mtindi(Yogurt)kama utakuwa nayo pakaa usoni na uache mchanganyiko ukifanya kazi kwa dk 15 baada ya hapo utanawa kwa maji ya uvugu vugu na kisha osha kwa maji ya barid yaliyotoka katika jokofu tumia mchanganyiko huo kwa muda wa wiki 2 utayafurahia matokeo.
No comments:
Post a Comment