Latest News

MUGABE AANZA KAMPENI ZA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2018

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe aanza kampeni za uchaguzi mkuu nchini unaotarajiwa kufanyika ifikapo mwaka 2018,aidhaRais Mugabe ameanza kampeni hizo akionekana kuwavutia zaidi vijana
Hapo Ijumaa rais Mugabe alianza kampeni zake kwa kutembelea eneo la Marondea, eneo ambalo linapatikana katika umbali wa kilomita 80 na jiji la Harare, amabapo Katika eneo hilo rais Mugabe alifanya kampeni katika uwanja wa Rudhaka.Katika eneo hilo rais Mugabe alifanya kampeni katika uwanja wa Rudhaka.


Licha ya kutuhumiwa kudhoofisha sekta ya kilimo baada ya kuwanyanganya wakulima wa kizungu mashamba, rais Mugabe amesema kuwa uchumi wa Zimbabwe unafanyiwa njama na mataifa ya Magharibi.
Rais Mugabe aliendelea kusema kuwa Zimbabwe sio taifa maskini na kuahidi kuwa katika sekta ya kilimo mavuno yataongezeka katika za ola Mahindi na Tumbaku.
Mugabe atakuwa mgombea wa kiti cha urais kupitia chama cha ZANU –PF katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika katikati ya mwaka 2018
Raisi ndiye raisi mzee zaidi barani Afrika,hivi karibuni amefanya sherehe ya kufurahia siku yake ya kuzaliwa ambapo alikuwa anatimiza miaka 93 na amekuwa madarakani tangu nchi hiyo ipate uhuru wake kutoka kwa wakoloni waingelez miaka ya 1980.

No comments:

Post a Comment

NAKUJUZA Designed by Templateism.com Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.
Published By Gooyaabi Templates