Latest News

SERIKALI YAJADILI UJENZI WA MRADI WA UZALISHAJI UMEME MTO RUFIJI.

Mhe. Rais Magufuli amekutana na timu ya wataalam wa masuala ya umeme na ujenzi wa miundombinu ya mabwawa ya maji kwa ajili ya kuzalisha umeme na kujadiliana nao kuhusu utekelezaji wa mradi mkubwa wa uzalishaji wa umeme katika maporomoko ya mto Rufiji (Stiegler’s Gorge Power Project) ambao una uwezo wa kuzalisha Megawatts 2,100 za umeme.

Mhe. Rais Magufuli amekutana na wataalamu hao ikiwa ni utekelezaji wa nia yake ya kuhakikisha mradi huo unaanza kujengwa haraka iwezekanavyo na kuzalisha umeme mwingi utakaosaidia kuharakisha maendeleo hapa nchini, hususani ujenzi wa viwanda.
“Kesho Waziri Mkuu wa Ethiopia Mhe. Hailemariam Desalegn anawatuma wataalamu wake waliojenga mradi mkubwa wa bwawa la maji la kuzalisha umeme kule Ethiopia, wakiwa hapa mtakutana nao na mtabadilishana uzoefu, nataka na sisi tusichelewe, tuzalishe umeme utusaidie kwenye ujenzi wa viwanda” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli

No comments:

Post a Comment

NAKUJUZA Designed by Templateism.com Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.
Published By Gooyaabi Templates