Jamii imetakiwa kuondokana na mtazamo hasi wa kuwa kuwaua watu wenye ualbino, kufukua makaburi yao na kuchukua viungo vyao ni kujipatia utajiri kwa kuwa mtazamo huo hauna ukweli wowote.
Kauli hiyo imetolewa na Muuguzi wa Idara ya Afya ambaye pia ni Mratibu lishe wa Wilaya ya Sengerema, Rachel Steven Ntogwisangu katika siku ya kimataifa ya kuongeza uelewa kuhusu watu wenye ualbino nchini ambapo ameitaka jamii kuwathamini watu wenye ualbino na kuachana na mila hizo potofu.
Rachel amewataka waganga wa jadi waone kuwa watu hao hawana hatia yoyote katika jamii kwani kuwafanyia vitendo hivyo vinawafanya waishi bila amani.
Kwa mujibu wa shirika la kimataifa la Amnesty International jumla ya watu 18 wenye ualbino wameuawa nchini Malawi na watano wametekwa nyara toka mwezi Novemba mwaka 2014.
Hata hivyo nchi kadhaa barani Afrika zimefanikiwa kudhibiti mauaji ya watu wenye ualbino wanaouawa kwa imani za kishirikina, vitendo ambayo vilikuwa vimekithiri kwenye nchi za Malawi, Tanzania na Msumbiji.
Na Veronica Martine, Sengerema.
No comments:
Post a Comment