Muslim Brotherhood yakataa shutuma za Saudi Arabia kwamba kundi hilo ni la kigaidi.
Siku ya Jumanne waziri wa mambo ya nje wa Saudi Arabia Adel al-Jubeir alitoa wito kwa Qatar kuwacha kuunga mkono makundi ya kigaidi huku akitoa mfano wa Muslim Brotherhood ya Misri na Hamas ya Palestina.
Waziri wa mambo ya nje Saudi Arabia |
Al Jubeir alitamka hayo akiwa ziarani Ufaransa na kusema kwamba hatua yake ya hivi karibuni ya kukata uhusiano wake na Qatar ilikuwa si kuleta madhara kwa nchi hiyo bali kuilazimisha Qatar kufanya chaguo lake kati ya Saudi Arabia ama kuunga mkono makundi ya kigaidi.
"Muslim Brotherhood inakana kwa kina na ghadhabu shutuma za viongozi wa Saudi Arabia dhidi yake." Kundi hilo lilifanya tangazo lake siku ya Jumatano.
Taarifa hiyo kutoka kundi hilo la Misri ilifahamisha kwamba Muslim Brotherhood imekuwa ikizingatia uhusiano mwema na mataifa ya ghuba na viongozi wake na hata kutoa huduma za kijamii,siasa,na uchumi.
Tangu kupinduliwa kwa serikali ya Mohammed Morsi kiongozi wa kundi la Muslim Brotherhood ,katika mapinduzi ya mwaka 2013 Saudi Arabia ,Misri na Milki za Kiarabu zilipiga marufuku kundi hilo.
No comments:
Post a Comment