Baada ya kuondokewa na nyota wake uongozi wa Mbao FC umesema hauna wasiwasi wowote na umeamua kuanza kutafuta vijana wengine katika mashindano ya Umisseta yanayoendelea Mwanza.
Add captioKikosi cha soka cha timu ya Mbao Sport club |
Mratibu wa timu hiyo Masalinda Njashi alisema tangu wanapanda daraja waliamua kutumia vijana wakiamini ndio wapambanaji katika timu, na hiyo ndio sababu ya wao kuendelea kuangalia vijana wengine katika mashindano hayo.
“Lengo letu sisi ni kutengeneza vijana tu kwahiyo baada ya hawa kuondoka tumeamua tuanze kuchukua vijana wengine katika Umisseta, wapo vijana wazuri wengi ambao tumewaona tutawachukua na tutawaweka katika kambi yetu kwa ajili ya msimu ujao,”alisema.
Akizungumzia kuhusu ripoti ya kocha wao Ettiene Ndayiragije alisema kuwa wanaitumia na ndiyo wanaifuata kwa sababu kocha huyo amekuwa na falsafa ya kutengeneza vijana na ndio maana amesisitiza tuongeze vijana.
“Tunatumia ripoti ya kocha wetu hatuwezi kuchukua wachezaji tu,kwa sababu tunaamini kuwa kocha wetu anarudi kikosini kwahiyo lazima tufate ripoti yake ambayo ameonyesha kuwa anahitaji vijana zaidi ya wazoefu katika timu na alitusisitiza tufanye hivyo na ndio maana tumekuwa wazito kusajili wachezaji wenye majina,”alisema.
Njashi aliongeza kuwa baada ya kufanya vizuri katika Kombe la Fa na ligi kiujumla zimeongezeka ofa za wadhamini ambao wanataka kuwa kujiunga katika msimu ujao kitu ambacho wanaimani kitaisaidia zaidi timu yao.
No comments:
Post a Comment