Ndege moja ya shirika la China Eastern Airlines ililazimika kurudi mjini Sydney Australia baada ya kupatwa na hitilafu wa mitambo ambayo ilisababisha shimo sehemu ya injini ya ndege hiyo.
Ndege ya MU736 ilikuwa safarini kutoka Sydney ikilekea Shanghai China lakini rubani akaripoti kuhusu matatizo kwenyr injini katibu saa moja baada ya ndege kuanza safari.,
Ndege ya shirika la China Eastern Airlines ikiwa imetua saama baada ya kupata hitilafu ikiwa angani |
Abiria waliambia vyombo vya habari kuwa walihisi harufu na kitu kinachochomeka ndani ya ndege.Ndege hiyo aina ya Airbus A330 ilitua salama na hakukuwa na ripti zozote za majeruhi.
Picha zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zilionyesha shimo kubwa upande wa injini.
No comments:
Post a Comment