Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Mh. Dk.Hamisi Kigwangalla mapema leo amempokea Samwel Mwanyika mwenye ugonjwa wa ‘Down Syndrome’ ama Utindo wa Ubongo au Mfanano kama wanavyojulikana, ambapo alishinda shindano la kimataifa la kupiga picha kwa vijana wenye utindio wa Ubongo maarufu kama “The Stephen Thomas Awards” lililofanyika nchini Uingereza hivi karibuni.
Akizungumza katika tukio hilo lililof
Ambapo Dk. Kigwangalla ameongeza kuwa, Serikali imefarijika kwa ushindi wa Samweli kwani umeleta heshima kubwa kwa Taifa.
“Serikali yatambua kazi nzuri iliyofanywa na Samweli. Hii inakuwa kama mafunzo kwa wengine kwani ameweza kuiletea heshima nchi yetu. Sisi tunatambua kazi nzuri iliyofanywa nae. Kwa wazazi wengine hii ni mafunzo katika kuwalea na kukuza vipaji vya watoto kama hawa”. Ameeleza Dk. Kigwangalla.
Kwa upande wake Mama Mzazi wa Samweli, Bi. Sophie Mshangama ameeleza kuwa, amefarijika kwa ushindi wa mwanae huku akiipongeza Serikali kwa ushirikiano mpaka kufika hatua ya mwanae kwenda kushiriki huko nje ambapo pia alipongeza Naibu Waziri wa Afya kwa hatua ya kuthamini na wanaishukuru Serikali kwa kila jambo.
No comments:
Post a Comment