Latest News

CHADEMA YA LAANI KUFUNGIWA KWA GAZETI LA MAWIO.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimelaani hatua ya serikali ya kulifungia gazeti la Mawio kwa muda wa miaka miwili kwa kosa la kuchapisha katika ukurasa wake wa mbele picha za Marais wastaafu ikiwahusisha na Sakata la Makinikia.

Wakati akizungumza na Waandishi wa Habari leo hapo jana Juni 16, 2017 jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mambo ya Nje Chadema, John Mrema amedai kuwa hatua hiyo ya serikali ni muendelezo wa kugandamiza uhuru wa vyombo vya habari.   
John Mrema. Mkurugenzi wa mawasiliano na mambo ya nje CHADEMA

“Tunalaani kufungiwa kwa gaz2eti la Mawio kwa sababu wamemjadili mkapa na kikwete, mbona tunamjadili Mwalimu Nyerere miaka yote na hakuna chombo cha habari kilichofungiwa kwa sababu hiyo,” amesema Mrema.
Gazeti la Mawio lilifungiwa na Waziri wa Habari, Dkt. Harrison Mwakyembe, ambapo alilisitisha kuchapisha nakala ngumu na au ya mtandaoni katika ipindi cha miezi 24 mfululizo

No comments:

Post a Comment

NAKUJUZA Designed by Templateism.com Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.
Published By Gooyaabi Templates