Latest News

MAMLAKA JIJINI LONDON YAONDOA WATU KATIKA MAJUMBA YA GHOROFA KWA KUHOFIA AJALI YA MOTO.

Kufuatia moto uliotokea katika jumba la Grenfell Tower,sasa mamlaka jijini London inahofia usalama wa moto katika majengo mengine kadhaa jijini humo.
Hatua hiyo inajiri ikiwa ni siku chache tu zimepita tangu kutokea kwa ajali ya moto katika moja ya ghorofa jijini humo na kupelekea vifo vya watu zaidi ya 76, na wengine kadhaa kujeruhiwa.
Wakaazi wa maeneo ya majumba ya ghorofa maeneo ya majengo ya Chalcots  wataondolea kutoka maeneo hayo kwa muda ili kufanyiwe ukaguzi wa kiwango cha usalama wa moto.
Wakaazi wa Chalcots walifahamisha kwamba wanahofia kuhusu hali ya usalama wa moto katika majengo wanatyoishi hasa baada ya watu 79 kufariki kwa moto katika Grenfell Tower hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment

NAKUJUZA Designed by Templateism.com Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.
Published By Gooyaabi Templates