Mwanamitindo maarufu kutoka Brazil Adriana Lima amefanya maonyesho ya nguo ya jukwaani mjini Antalya nchini Uturuki.
Kwa mujibu wa habari,Adriana ndie aliyeongoza maonyesho ya nguo usiku huo na alikuwa kivutio kikubwa kwa watazamaji.
Mwanamitindo Adriana Lima |
Mwanamtindo huyo alilitawala jukwaa kwa kuvaa nguo nne tofauti usiku wa maonyesho ya Dosso Dossi.
Wanamitindo maarufu wengine kutoka Brazil kama Isabeli Fontana, Ana Beatriz Barros, Izabel Goulart walikuwa gumzo katika maonyesho hayo.
Mwanamuziki Ayşe Hatun Önal alimalizia hafla hiyo kwa kutumbuiza jukwaani
No comments:
Post a Comment