Latest News

BUNGE LAAZIMIA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA RAISI MAGUFULI

Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamepitisha azimio la kumpongeza Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa hatua alizochukua kukabiliana na upotevu wa mapato ya serikali katika sekta ya madini nchini.
Azimio hilo limeonesha kuwa Bunge lipo tayari kutoa ushirikiano wa dhati kwa kadri itakavyohitajika katika kuhakikisha juhudi, uthubutu na uzalendo aliouonesha Rais Magufuli haupotei bure bali unakuwa chachu ya kuhakikisha kuwa sekta ya madini inachangia katika kuleta maendeleo kwa wananchi na taifa kwa ujumla.
Bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania

No comments:

Post a Comment

NAKUJUZA Designed by Templateism.com Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.
Published By Gooyaabi Templates