Latest News

GOOGLE YALIPISHWA MABILIONI YA DOLA NA TUME YA ULAYA.

Google imepigwa faini ya ya dola bilioni 2.7 na tume ya ulaya baada ya tume hiyo kuamua kuwa Google ilikuwa imekiuka mamlaka yake ya kuweka matangazo yake binafasi kuwa ya kwanza.
Faini hiyo ndiyo kubwa zaidi iliyotolewa na tume ya ulaya hadi leo, kwa kampuni ambayo imelaumiwa kwa kukiuka sheria za biashara. Amri hiyo pia inataka Google kundoa vizingiti vinavyozuia ushindani ndani ya kipindi cha siku 90 la sivyo ichukuliwe hatua zaidi.
Hata hivyoampuni hiyo ya Marekani inasema huenda ikakata rufaa.
Matangazo ya Google huonekana kwanza pindi mtu anapokuwa anatafuta kitu kwenye mtnandao huo, muda mwengine husukuma pembeni matangazo mengine yasiyo ya Google.
Tume ya Ulaya ilisema inaiachia Google jukumu la kuamua ni mabadiliko yapi itafanyia mifumo yake ya mauzo. "Kile ambacho Google imekifanya na haramu chini ya sheria za EU," alisema Margrethe Vestager, kamishina wa ushindanii wa kibiashara wa tume ya EU


Tume ya Ulaya imekuwa ikichunguza mifumo ya bioshara ya GoUchunguzi huo ulianza kufuatia malalamiko kutoka makampuni kama Microsoft miongoni mwa mengine.
Bi Margrethe Vestager. Kamishina wa ushindanii wa kibiashara wa tume ya EU


    Tume ya Ulaya imekuwa ikichunguza mifumo ya bioshara ya Google tangu mwaka 2010
    Uchunguzi huo ulianza kufuatia malalamiko kutoka makampuni kama Microsoft miongoni mwa mengine.

    Hata hivyo Microsoft hajatoa tamko lolote kufuatia uamuzi huo baada ya mahasimu hao kufikia makubaliano ya kujaribu kuzuia kesi mahakamani siku za usoni

    No comments:

    Post a Comment

    NAKUJUZA Designed by Templateism.com Copyright © 2014

    Theme images by Bim. Powered by Blogger.
    Published By Gooyaabi Templates