Latest News

AKUTWA AMEUAWA NA WATU WASIOJULIKANA.



Mlinzi wa kampuni ya Museco  anaekadiliwa kuwa na umri wa 34 mkazi wa kijiji cha Ibondo kata ya Ibondo wilayani Sengerema amekutwa ameuawa na watu wanaodhaniwa kuwa ni wezi katika eneo la kazi.

Mwenyekiti wa mtaa wa Migombani, Jane Musoga ambapo tukio hilo lilipotokea alithibisha kutokea kwa  tukio hilo na kudai kuwa tabia ya kuuawa walinzi imeshamili kwa kasi wilayani hapo na alimtaja mlinzi huyo kuwa Juma Msafiri Fugunya mkazi wa Ibondo wilayani humo.
“Mimi sielewi nini kimewakumba wanasengerema kwani matukio haya yanazidi kutokea kila mara wananchi wangu nawaombeni tushirikiane kwa pamoja na jeshi la polisi kufuatilia chanzo cha matukio haya kwa hali hii huwezi kuishi kwa amani hivyo tutafuteni suluhu yake,” alisema Mwenyekiti wa Mtaa huo.
Nao walinzi waliliomba Jeshi la Polisi wilayani hapo kufanya ufuatiliaji wa matukio hayo yanayoendelea kutokea kwa baadhi ya walinzi kwani mpaka sasa wanafanya kazi kwa kuhofia usalama wa maisha yao.
“Jamani sisi walinzi ni wananchi wenzenu kwa nini mnatufanyia vitendo vya kinyama namna hii kwa sasa imefikia hatua tunaenda kazini usiku tukiwaza kuwa leo sijui zamu ya nani kuuawa tunaelekea wapi serikal na wananchi wenzetu tusaidieni kwani mpaka sasa hata siku hazijapita kauawa mwingine,” alisema Walinzi.
Kwa upande wake mmiliki wa Mgahawa wa pombe wa Resepect Glocery Thobias Mussa mwenye umri wa miaka 41 ambapo mlinzi huyo ameuawa amesikitishwa na tukio hilo na kudai kuwa hii ni mara ya pili tukio kutokea katika Mgahawa wake.
“Sijui tukio hili limetokea vipi kwa sababu nimepigiwa simu asubuhi ndiyo nikaelezwa kuwa mlinzi wangu Juma Fugunya cha ajabu zaidi watu hawa waliomuua hawajachukua kitu chochote tofauti na uhai wake,” alisema Mussa.
Jeshi la polisi wilayani Sengerema limefika eneo la tukio na kuuchukua mwili wa marehemu kisha kuupeleka katika Hospitali teule ya wilaya ya Sengerema kwa ajili ya kuuhifadhi na baadae utasafirishwa hadi kijiji kwao marehemu kwa ajili ya maziko.
Mkuu wa wilaya ya SengeremaMkaoni Mwanza Mh;Emmanuel Kipole alilaani vikali tukio hilo.
Na Veronica  Martine    Sengerema

No comments:

Post a Comment

NAKUJUZA Designed by Templateism.com Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.
Published By Gooyaabi Templates