Kuna ripoti tofauti kuhusu ni wafungwa wangapi walifanikiwa kutoroka.
Redio inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa Radio Okapi, inasema kuwa wafungwa 17 walitoroka, wengi kutoka kwa kituo cha polisi
Mtandao mmoja wa habari nchini Congo wa Politico, unasema kuwa washambuliajia walikuwa ni wanachama wa Bunda dia Kongo ambalo ni kundi la dini lililo na mtazamo wa siasa.
Serikali inalilaumu kundi hilo kufuatia shambulizi lililotokea katika gereza kuu la Kinshasa mwezi uliopita ambapo mamia au hata maelfu ya wafungwa walitoroka.
No comments:
Post a Comment