Latest News

RAISI MUGABE AMFUTA KAZI MUENDESHA MASHTAKA WA ZIMBABWE.

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amemfuta kazi mkuu wa mashtaka wa nchi hiyo Jonannes Toanana, baada ya jopo la uchunguzi kumpata na hatia ya ukosefu wa nidhamu na uzembe.
Rais Robert Mugabe
Raisi wa Zimbabwe Robert Mugabe.
Bwana Tomana ambaye wakati mmoja alikuwa mshirika mkubwa wa Rais, alisimamishwa kazi mwezi Februari mwaka uliopita.
Aliondolewa ofisini baada ya kutupilia mbali mashtaka dhidi ya wanaume wawili waliodaiwa kupanga njama ya kulipua kiwanda cha maziwa kinachomilikiwa na mke wa Rais Mugabe.
Vyombo vya habari saa vinasema kuwa Tomana sasa atajibu mastaka kwenye mahakama ya juu kwa makosa ya matumizi mabaya ya mamlaka.

No comments:

Post a Comment

NAKUJUZA Designed by Templateism.com Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.
Published By Gooyaabi Templates