Latest News

DIEGO COSTA AISIKILIZIA CHELSEA KUJUA HATMA YAKE KLABUNI HAPO.

LONDON, ENGLAND.Mshambuliaji Diego Costa amewaachia Chelsea wajikaange wenyewe kuhusu hatima yake kwenye kikosi hicho cha Stamford Bridge.

Staa huyo hivi karibuni alitumiwa meseji na kocha Antonio Conte akiambiwa hahitajiki tena kwenye kikosi hicho kwa sababu hayupo kwenye mipango ya Mtaliano huyo.
Na sasa, fowadi huyo ambaye alihusika kwenye mabao 27 katika Ligi Kuu England msimu uliopita, amelichukulia suala hilo la kocha wake kuwa ni kubwa na tafsiri yake ina maana aanze kutafuta timu ya kuichezea msimu ujao.
Diego Costa

Lakini, sasa amesema kila kitu kitaamriwa na Chelsea wenyewe baada ya kusema hivi: “Nina mkataba wa miaka miwili klabuni Chelsea, kwa hivyo wao ndiyo wenye kufanya uamuzi. Kwa sasa nimekaa tu nasubiri uamuzi utakaochukuliwa na klabu.”
Kutokana na hilo, Costa sasa anajiandaa kukutana na maisha tofauti nje ya Chelsea na mipango inadaiwa kwamba staa huyo anaweza kwenda kujiunga na klabu yake ya zamani ya Atletico Madrid  baada ya kudai anafurahia maisha ya Madrid.
Staa huyo pia anawindwa na klabu za kutoka China na kama dili likigoma la kurudi Madrid basi anaweza kutimkia China kama Chelsea itaamua kumfungia milango moja kwa moja

No comments:

Post a Comment

NAKUJUZA Designed by Templateism.com Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.
Published By Gooyaabi Templates