Latest News

MALI YAHIMIZA KUUNDWA KWA KIKOSI CHA KUPAMBANA NA UGAIDI.

Waziri wa mambo ya kigeni nchini Mali jana Ijumaa amelishinikiza Baraza la   Usalama la Umoja wa Mataifa kupitisha haraka azimio la kuundwa kikosi maalum kwa ajili ya kupambana makundi ya kijihadi ambayo yanazidi kukabili nchi hiyo ya ukanda wa Sahel.

                                            Waziri, Abdoulaye Dio ameelezea wasiwasi mkubwa wa Rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keita, ambaye anaongoza muungano wa kikanda wa nchi tano zinazojulikana kama G5 za ukanda wa Sahel,kuhusu ugumu unaochelewesha kuidhinishwa kwa azimio hilo. Amewataka wajumbe wa umoja huo kupitisha azimio hilo bila kuchelewa.
Abdoulaye Diop:Waziri wa mambo ya nje nchini Mali.

Kundi la G5 linalojumuisha nchi za Mali , Chad, Mauritania na Burkina Faso, zilikubaliana mwezi Machi kuunda kikosi imara cha askari elfu tano ili kukabiliana na wanajihadi lakini linangoja idhini ya Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa kabla ya kutekeleza azma hiyo.

No comments:

Post a Comment

NAKUJUZA Designed by Templateism.com Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.
Published By Gooyaabi Templates