Mamlaka za Milki za kiarabu zatangaza kuwa raia watakaovaa jezi za Barcelona zilizobeba jina na Qatar wataweza kuhukumiwa miaka 15 jela.
Mashabiki wa soka kutoka Milki za Kiarabu watajiingiza matatani wakivalia t- sheti za klabu ya Barcelona zilizo na lebo ya Qatar Airways.
Hivi karibuni kumekuwa na mvutano mkubwa wa kidiplomasia kati ya Qatar na majirani zake wa nchi za Ghuba wakiishutumu Qatar kulifdhili kundi la kigaidi la Muslim britherhood la Misri. |
Aidha mamlaka hiyo ilifaamisha pia watakapatikana na hatia hiyo watakatwa faini ya takriban dola elfu 135 au jela miaka 15.
Mnamo mwaka 2011 idara ya uwekezaji ya michezo ya Qatar ilifanya mkataba na klabu bingwa ya kimataifa ya Barcelona na kutengeneza jezi za timu hiyo iliyobeba jina la Qatar Airways .
Klabu hiyo ya Uhispania ni maarufu na inapendwa sana katika mataifa ya Ghuba ya kiarabu na uamuzi huo ulizua hasira baina ya mashabiki walioelezea hisia zao kupitia mitandaoni.
No comments:
Post a Comment