Latest News

MABAKI YA BINADAMU YAPATIKANA MIAKA KUMI BAADA YA KUTOWEKA KWAKE.

Mabaki ya binadamu yamepatiakana katika kichaka kikubwa nchini Australia ya mwanamume ambaye alitoweka miaka 10 iliyopita.
Matthew Leveson, ambaye alikuwa na umri wa miaka 20, alionekana mara ya mwisho akiondoka katika klabu moja mjini Sydney mwaka 2007, akiwa na rafiki yake Michael Atkins.
Bwana Atkins aliondolewa mashtaka ya mauaji ya bwana Leveson mwaka 2009.
Baadaye alipata makubaliano ya kuzuia kufunguliwa mashtaka ikiwa angetoa habari za ulipo mwili wa Leveson.
New South Wales search for human remains, 2 JuneHaki miliki ya pichaEPA
Image captionPolisi waiktafuta mabaki
Polisi walipata mabaki hayo katika bustani ya Sydney siku ya Jumatano. Uchunguzi wa DNA ulibainisha kuwa mabaki hayo yalikuwa ni ya bwana Leveson.
Wazazi wake, Faye na Mark Leveson waliweka maua eneo hilo wiki iliyopita.
"Tumepigana kwa muda wa maika tisa unusu hadi kufika siku hii na kumleta mtoto wetu nyumbani," Bwana Leveson aliwaambia waandishi wa habar.
NA: BBC SWAHILI

No comments:

Post a Comment

NAKUJUZA Designed by Templateism.com Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.
Published By Gooyaabi Templates