Shanghai, China. Mshambuliaji Carlos Tevez amekiriki anataka kuachana na soka la China 'Chinese Super League' ikiwa ni miezi sita tangu aliposaini kwa uhamisho uliovunja rekodi pamoja na kulipwa mshahara wa pauni 615,000 kwa wiki.
Carlos Tevez |
Tevez (33) aliachana na klabu yake ya Boca Juniors Desemba mwaka jana baada ya kusaini mkataba na Shanghai Shenhua.
Lakini baada ya kufunga bao moja katika michezo sita, Tevez amesema ataondoka CSL wakati msimu huu utakapokwisha Septemba.
Shanghai ipo juu kwa pointi nne katika timu zilizokuwa katika janga la kushuka daraja baada ya kucheza mechi 11, na nyota huyo wa zamani wa Manchester United, Manchester City, West Ham na Juventus akidai kuwa hakutaka kucheza soka Mashariki ya Mbali kama chaguo lake la kwanza.
Tevez aliimbia TyC Sports: “Niliondoka si kwa sababu ya kuiumiza Boca. Kusema ukwli sijui nini kitakachotokea mwisho wa mwaka huu.
“Kama nina lengo la mafanikio, ni vigumu kubaki katika klabu hii. Natakiwa kurudi nyuma, najua nimefanya kila kitu hapa.
No comments:
Post a Comment