Mahakama nchini Brazil imemuhukumu gavana wa zamani wa jimbo la Rio de Janeiro Sergio Cabral, miaka 14 gerezani kwa kuhusika katika rushwa na utakatishaji wa fedha.
Cabral anatajwa kuhusika kwenye upokeaji wa mamilioni ya dola katika miaka nane aliyokuwa madarakani. Fedha hizo ni sambamba na zile za makampuni yaliyopata mkataba wa kujenga miundombinu wakati wa michuano ya Olimpiki.
|
Bw. sejio Cabral, aliyekuwa gavana wa jimbo la Reo de Janeiro nchini Brazil |
Jaji Sergio Moro ambaye ndiye aliyetoa hukumu hiyo amesema hakuna ushahidi wa kutosha kama mke wa Cabral aitwaye Adriana Ancelmo ambaye pia ni mwanasheria maarufu nchini humo alihusika.
|
Jaji Sergio Moro |
No comments:
Post a Comment