Latest News

KOREA YAMUACHIA HURU MFUNGWA MMAREKANI.

Korea Kaskazini imemwachilia huru mwanafunzi Mmarekani Otto Warmbier ambaye alikuwa amefungwa jela katika taifa hilo la bara Asia, waziri wa mambo ya nje wa Marekani amesema.
Bw Warmbier, 22, alihukumiwa kufungwa jela miaka 15 na kazi ngumu Machi 2016 baada ya kupatikana na hatia ya kujaribu kuiba bango la propaganda kutoka kwenye hoteli moja.
Otto Wambier akiwa chini ya ulinzi nchini Korea ya Kaskazini
Bw Tillerson amesema Bw Warmbier sasa yuko njiani kurejea Marekani ambapo ataungana tena na jamaa zake Cincinnati, Ohio.
Gazeti la Washington Post limemnukuu babake Fred akisema mwanawe wa kiume amesafirishwa kama mgonjwa wka sababu hana fahamu.
Gazeti hilo linasema wazazi wa Warmbier waliambiwa mwana wao wa kiume alianza kuugua ugonjwa wa botulism, ugonjwa nadra ambao humfanya mtu kupooza, muda mfupi baada ya kesi yake kumalizika miezi 15 iliyopita.
Alipewa dawa za kumfanya alale, na tangu wakati huo hajawahi kupata fahamu tena.
"Mwana wetu anarejea nyumbani," Fred Warmbier amenukuliwa akisema.
"Kwa sasa, tunachukulia hiki kuwa kisa cha ajali tu. Tutamuona tena mwana wetu Otto leo usiku."

Alilazimishwa kukiri mashtaka?

Otto Warmbier, mwanafunzi aliyekuwa amehitimu na shahada ya uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Virginia, alikuwa amezuru Korea Kaskazini kama mtalii akiwa na shirika la Young Pioneer Tours alipokamatwa 2 Januari 2016.
Alitoa hotuba kwenye televisheni akikiri mashtaka mwezi mmoja baadaye, ambapo alisema kwamba alikuwa amekusudia kubeba bango hilo kama "kumbukumbu" kwa kanisa moja la Marekani.
Aliongeza kuwa "lengo langu lilikuwa kudhuru moyo na kujitolea kwa watu wa Korea kufanya kazi.
Haijabainika iwapo alitoa hotuba hiyo kwa hiari au alilazimishwa.
Hata hivyo, wafungwa kutoka nchi za nje nchini Korea Kaskazini wamekuwa mara kwa mara wakikana taarifa walizozitoa wakikiri makosa, wakisema kwamba walishinikizwa kutoa hotuba hizo.
Baada ya kesi iliyodumu mdua mfupi 16 Machi, Bw Warmbieri alihukumiwa kufungwa jela miaka 15 na kufanyishwa kazi ngumu.
Wazazi wake Fred na Cindy waliambia CNN mapema mwezi huu kwamba walikuwa hawajawasiliana na mwana wao kwa zaidi ya mwaka mmoja.
Walieleza wasiwasi wao kuhusu hatima yake hasa baada ya uhasama kati ya Korea Kaskazini na Marekani kuzidi kutokana an hatua ya Pyongyang kufanyia majaribio makombora ya masafa marefu.
Meli za kivita za Marekani zilitumwa eneo hilo.
Bw Warmbier ameachiliwa saa chache baada ya nyota wa mpira wa kikapu wa Marekani Dennis Rodman kutua Korea Kaskazini.
Haijabainika iwapo matukio hayo mawili yana uhusiano wowote.
Bw Rodman ni rafiki wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un na amezuru nchi hiyo mara kadha miaka ya karibuni.
Alisema amezuru taifa hilo kama raia binafsi, na "lengo langu ni kuona iwapo ninaweza kuleta michezo hapa Korea Kaskazini".
Raia wengine watatu wa Marekani bado wanazuiliwa Korea Kaskazini.
Kim Dong-chul, 62, mmishenari wa Marekani mwenye asili ya Korea, Profesa Mmarekani mwenye asili ya Korea Kim Sang-duk (auTony Kim); naKim Hak-song, aliyekuwa akifanya akzi Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Pyongyang (PUST).

No comments:

Post a Comment

NAKUJUZA Designed by Templateism.com Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.
Published By Gooyaabi Templates