Muungano wa upinzani nchini Kenya wailaumu serikali kufuatia ukosefu wa unga nchini
Raisi wa Kenya Uhuru Kenyata. |
Kiongozi wa muungano wa upinzani wa NASA nchini Kenya Raila Odinga amesema kuwa ukosefu wa unga wa mahindi nchini Kenya ometokana na serikali ya Uhuru Kenya kupuuza onyo iliotolewa na makampuni yanayohusika na usagaji wa mahaindi mwaka 2016.
Odinga amesema kuwa hatua iliochukuliwa na Serikali ya Kenya inazidisha madhara ya njaa kwa kuwa mahindi kutoka Mexico hadi kufika Kenya huchua muda wa zaidi ya siku 40.
Odinga amemtaka rais Uhuru Kenyetta kusafiri kwa dharura nchi Ethiopia kununua mahindi kwa kuwa usafirishaji wa Mahindi kutoka Ethiopia kuelekea Kenya huchukua siku mbili pekee.
No comments:
Post a Comment