Mikono, viganja na vidole ni kati ya sehemu muhimu katika mwili wa msichana. Mikono hutumika kufanya shughuli nyingi za nyumbani, shuleni na sehemu mbalimbali katika maisha kuanzia kutandika kitanda, kupika, kufanya usafi, kuandika, kujiremba pamoja na majukumu mengine mengi. Mikono isipotunzwa vizuri ni rahisi sana kuharibika, kupoteza mvuto wake wa asili na kuharibu afya ya kucha. Hitaji la urembo wakati mwingine humsukuma msichana katika matumizi ya vipodozi vya kupaka kwenye kucha zake ili kukamilisha urembo wake.
Urembo wa vidole na kucha sio lazima ufanyike katika saluni au kwa wataalamu wa kupamba kucha, msichana anaweza kushughulikia afya na urembo wa vidole na kucha zake kwa gharama nafuu na kwa muda ambao mwenyewe anaona unafaa kufanya hivyo hata akiwa nyumbani. Hii pia itamsaidia Msichana kuchagua vipodozi salama kwa afya ya kucha zake na mwili kwa ujumla. Ni jambo la muhimu kufahamu kuwa baadhi ya vipodozi vinavyotumika katika urembo wa kucha, vina rangi na sumu zisizofaa kwa afya. Sumu kama vile ‘Formaldehyde na Toluene’ zinazopatikana katika baadhi ya rangi za kucha zina madhara kwa afya ya msichana.
Ni kweli kuwa kucha nzuri huongeza urembo, mvuto na furaha ya msichana lakini pia ni busara kukumbuka kuwa afya ni muhimu kuliko urembo na uzuri. Afya ya mwili na kucha za msichana kwa ujumla hutegemea chakula bora chenye protein, madini na vitamini na siyo rangi na vipodozi.
Upungufu wa vitamini A, B Complex, proteni, madini ya chuma na chokaa (kalishiamu) mwilini husababisha kucha zipoteze afya yake ya asili. Kucha ambazo hazina afya zinaweza kuoza, kukauka, kupinda, kupasuka au kuwa na umbo kama kijiko. Magonjwa ya kuvu (fungus), na baadhi ya dawa za kupunguza makali ya virusi pia huharibu afya ya kucha. Mojawapo ya athari za dawa za kupunguza makali ya VVU aina ya Zidovudine (ZDV) ni kucha kuwa na rangi nyeusi.
Kwa ajili ya afya bora ya kucha msichana anashauriwa kula mboga za majani, maharage, korosho, asali na matunda kwa wingi kila siku. Usafi wa kucha kila siku kwa kuziosha kwa maji ya uvuguvugu na sabuni laini pamoja na brashi ndogo ya mikono huimarisha afya ya kucha. Kucha pia zinaweza kusafishwa kwa maji ya mmea wa mshubiri (Aloevera), kitunguu saumu kilichopondwa pondwa au kitunguu maji kisha viganja na vidole vikaushwe vizuri na kupaka losheni.
Kucha za msichana zinatakiwa zisiwe ndefu ili kuepuka utunzaji wa vimelea vinavyosababisha magonjwa na kurahisisha utunzaji na usafi wa kucha. Kucha ndefu zinaweza kuwa chanzo cha hatari kwa afya ya msichana na familia yake hasa pale msichana anapohusika na uandaaji wa chakula cha familia. Katika familia nyingi, hasa familia za kiafrika wasichana ndio wanaobeba wajibu na majukumu ya kuandaa chakula cha familia.
Kwa afya nzuri ya kucha, msichana anashauriwa kukata kucha zake ili ziwe fupi kadri anavyotaka kwa kutumia ‘nail cutter’ au mkasi mdogo au wembe mpya ambao haujatumiwa na mtu mwingine. Kuchangia nyembe za kukatia kucha si salama kwani kunaweza kuwa njia mojawapo ya kusambaza vimelea vya magonjwa hatari ya kuambukiza kama vile virusi vinavyosababisha UKIMWI na ugonjwa wa homa ya ini.
Ni vizuri kulainisha ncha za kucha baada ya kuzikata kwa kutumia tupa ya kucha (nail file) na kuzisugua kuelekea upande mmoja ili kuepuka kucha zisivunjike au zisisababishe michubuko ya ngozi wakati wa kujikuna. Kusugua kucha kwa kwenda mbele na nyuma kunaweza kusababisha kucha zivunjike kwa urahisi na haraka.
Kwa afya njema ya kucha, msichana pia anashauriwa asifungue pini za barua au kukwangua vocha za simu kwa kutumia kucha. Kucha zisikatwe kwa kutumia meno na zisilowekwe kwenye maji kwa muda mrefu hasa pale maji hayo yanapokuwa na kemikali au sabuni. Kwa ajili ya afya njema ya kucha za miguuni, ni muhimu kuhakikisha kuwa, viatu kabla ya kuvaliwa vinakuwa vikavu na safi kabisa. Viatu visipotumiwa pia vihifadhiwe sehemu kavu isiyo na vumbi, maji au unyevunyevu ili kuepusha visiwe makazi ya kuvu (fungus
Recent Posts
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Follow us on facebook
Popular Posts
-
Uzuri wa ngozi sio rangi tu bali ni muonekano wa ngozi yenyewe kwamba ina afya na mng'ao unaoashiria afya njema. Leo tushirikishane ji...
-
Wapiganaji wa Boko Haram wamefanya mashambilizi makali katika mji ulioko kaskazini mashariki mwa Nigeria. Watu walioshuhudia wanase...
-
Mikono, viganja na vidole ni kati ya sehemu muhimu katika mwili wa msichana. Mikono hutumika kufanya shughuli nyingi za nyumbani, shuleni na...
-
Lipstick ni aina ya vipodozi vyenye rangi mbalimbali vinavyotumika kupaka katika midomo hasa ya wanawake ili kuongeza urembo na mvuto wao. ...
-
Asalaam akeykum warahmatullah wabarakatu.na pia niwasalim na ndugu zangu katika Adam kwa kusema Tumsifu yesu kristo Leo tutaangalia nafa...
-
Rais wa Nigeria amepigwa picha akiwa mjini London kwa mara ya kwanza tangu andoke nchini mwake karibu siku 80 zilizopita. Rais Muhamm...
-
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na watoto, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi Kigwangalla ameshiriki futari maalum iliyoandaliwa ...
-
Mlinzi wa kampuni ya Museco anaekadiliwa kuwa na umri wa 34 mkazi wa kijiji cha Ibondo kata ya Ibondo wilayani Sengerema amek...
-
Mshambuliaji wa zamani wa Simba, Daniel Sserunkuma amekamilisha uhamisho wake wa kujiunga na klabu ya Ittihad Riadi Tanger inayoshiriki l...
-
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamepitisha azimio la kumpongeza Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano ...
Side Ad
Blog Archive
-
▼
2017
(104)
-
▼
June
(100)
- MAWAKILI 248 WAAPISHWA DAR
- DOKTA KIGWANGALA AMPOKEA SAMWEL NA KUMPONGEZA.
- MTOTO WA MIAKA MITANO AIBIWA MWANZA.
- KATIBU MKUU WA TFF AMTEMBELEA NAHODHA WA SERENGETI...
- SSERENKUMA WA SIMBA APATA SHAVU MOROCO.
- USAIN BOLT KUSTAAFU MWAKANI.
- EVERTON MBIONI KUMNYAKUA MNIGERIA HENRY ONYEKURU.
- NYUKI WAMPELEKA MTUHUMIWA POLISI.
- CHINA YA ILAUMU INDIA KWA UVAMIZI.
- LOWASA AHOJIWA NA POLISI.
- GOOGLE YALIPISHWA MABILIONI YA DOLA NA TUME YA ULAYA.
- SERIKALI YAJADILI UJENZI WA MRADI WA UZALISHAJI UM...
- BRN YAZIKWA RASMI.
- SERIKALI KUONGEZA KASI YA ULINZI DHIDI YA UHALIFU ...
- FABINHO AKARIBISHA MUALIKO WA MANCHESTER UNITED
- SHAMBULIO LA BOMU LATOKEA SAUDIARABIA KARIBU NA MS...
- MAMLAKA JIJINI LONDON YAONDOA WATU KATIKA MAJUMBA ...
- RAISI WA MISRI ABDEL FATTAH ATOA MSAMAHA KWA WA FU...
- TAASISI ZA KIFEDHA ZAOMBWA KUWEKEZA NA VIJIJINI.
- MAKAMU WA RAISI SAMIA SULUHU AWATAKA WAWEKEZAJI WA...
- MOTO WAATHIRI HUDUMA YA NISHATI YA UMEME, NKASI MK...
- KAULI YA RAISI MAGUFULI KUHUSU UJAUZITO MASHULENI ...
- KOREA KASKAZINI YAFANYA MAJARIBIO YA KURUSHA MAKOM...
- QATAR YAPEWA MASHARTI NA MAJIRANI ZAKE
- TRUMP AILAUMU KOREA KASKAZINI KWA KUSABABISHA KIFO...
- UMITASHUMTA KUANZA KUTIMUA VUMBI JUMAPILI HII
- CARLOS TEVES ACHEMSHA CHINA.
- WADAU WA SOKA WALIA NA MALINZI
- AFISA MTENDAJI MBARONI KWA KUPOKEA RUSHWA.
- MKUU WA WILAYA AWAAGIZA MAWAKALA KUTUMIA MIZANI SA...
- CHADEMA YA LAANI KUFUNGIWA KWA GAZETI LA MAWIO.
- DOKTA KIGWANGALA AHIMIZA UPENDO NA USHIRIKIANO KWA...
- SERIKALI KUPANDA MITI ILI KUKABILIANA NA HALI YA J...
- AFRIKA KUSINI YAADHIMISHA MIAKA 41 TANGU KUTOKEA K...
- ALIYEKUWA KANSELA WA UJERUMANI AFARIKI DUNUIA
- SHAMBULIO LA BOMU LAUWA WATU WA NNE KENYA.
- TRUMP ABANWA TENA NA MAHAKAMA.
- MALI YAHIMIZA KUUNDWA KWA KIKOSI CHA KUPAMBANA NA ...
- HOSPITALI TEULE SENGEREMA YA KABILIWA NA UHABA WA ...
- TANESCO YAWATAHADHARISHA WANANCHI NA VISHOKA WA AJIRA
- SERIKALI YAJIPANGA KUDHIBITI MAGONJWA YALIYOSAHAUL...
- JAMII YATAKIWA KUACHANA NA MILA POTOFU DHIDI YA WA...
- SERIKALI YAVIONYA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU SAKATA ...
- BUNGE LAAZIMIA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA RAISI MAGUFULI
- ACASIA KUILIPA TANZANIA
- RAISI WA UTURUKI RECEP ERDOGAN AKOSOA MSIMAMO WA N...
- RONALDO KUSHTAKIWA KWA KUKOSA KULIPA KODI.
- IRAN NI YA PILI KUFUZU TIKETI YA KUSHIRIKI KOMBE L...
- KIMBUGA CHA ATHIRI USAFIRI WA ANGA HONG KONG
- MOROKO YAUNGANA NA QATAR.
- AHUKUIWA JELA MIAKA 15 KWA UFISADI.
- KOREA YAMUACHIA HURU MFUNGWA MMAREKANI.
- AZAM,SIMBA NA YANGA ZAZIDI KUIBOMOA MBAO FC
- MBAO: BADO TUPO VIZURI.
- DIEGO COSTA AISIKILIZIA CHELSEA KUJUA HATMA YAKE K...
- MDEE NA BULAYA KUIBUKIA MAHAKAMANI
- MWANAMITINDO KUTOKA BRAZIL ADRIANA LIMA AFANYA MAO...
- FIFA YAIKINGIA KIFUA QATAR
- MGOGORO WA KIDIPOMASIA KATI YA QATAR NA MAJIRANI Z...
- AASKALI AUAWA KATIKA SHAMBULIZI LA LIGAIDI SAUDIAR...
- NDEGE YA CHINA YATUA SALAMA BAADA YA KUPATA HITILA...
- SERIKALI YA LIBYA YAKASRISHWA NA KUACHIWA HURU KW...
- UZEMBE SEKTA YA MADINI WALISABABISHIA TAIFA HASARA...
- USAIN BOLT KUSTAAFU RIADHA.
- MANCHESTER UNITED WAANZA NA MLINZI WA BENIFICA
- WAANDAMANA WAKIDAI HAKI ZA WAPENZI WA JINSIA MOJA.
- ZAIDI YA WAHAMIAJI 100 WAKAMATWA NCHINI MEXICO
- MAREKANI YASHAMBULIA NGOME YA AL SHABABY.
- WAFUNGWA WENGINE 930 WATOROKA GEREZANI NCHINI KONG...
- NDONDO CUP KUANZA KUTIMUA VUMBI MWISHONI MWA WIKI.
- AKUTWA AMEUAWA NA WATU WASIOJULIKANA.
- WADUDU WAHARIBU SOKO LA MBOGA ZA MAJANI GEITA.
- AISHI MANURA ATUA MSIMBAZI.
- RAISI MUGABE AMFUTA KAZI MUENDESHA MASHTAKA WA ZIM...
- MAREKANI YAZIHAKIKISHIA USALAMA NCHI WANACHAMA WA ...
- JINAMIZI LA KUTOROKA KWA WAFUNGWA LAENDELEA KUIAND...
- MAREKANI YAIOMBEA SALAMA QATAR DHIDI YA MAJIRANI Z...
- MWAMBUSI AFUNGUKA KILICHO IUMIZA YANGA DHIDI YA AF...
- ASALI NA UREMBO WA SULA YAKO.
- MANCHESTER UNITED YAMUWEKA NJIAPANDA ZLATAN IBRAHM...
- MESSI ANA NDOTO YA KUZEEKEA BARCELONA
- COMEY AWEKA HADHARANI KILICHOMFANYA ATUMBULIWE NA ...
- SERIKALI YATANGAZA ORODHA YA WATAKAO JIUNGA KIDATO...
- WIZI WA SAMANI WATISHIA KUHARIBU URITHI WA DUNIA.
- UHABA WA UNGA KENYA WAMUWEKA LAWAMANI KENYATA
- AHUKUMIWA MIAKA 35 JELA KWA KUIKOSOA FAMILIA YA KI...
- MUSLIM BROTHERHOOD YAKEMEA VIKALI SHUTMA ZA UGAIDI...
- TEAM YA TAIFA YA SOKA YA TANZANIA[TAIFA STARS] KUR...
- GOR MAHIA YATINGA FAINALI YA SPORT PESA.
- UFINYU WA MVUA NA HALI YA KUONGEZEKA KWA JOTO VYA ...
- BARA LA ASIA KUKABLIANA NA UCHAFUZI WA MAZINGIRA B...
- MABAKI YA BINADAMU YAPATIKANA MIAKA KUMI BAADA YA ...
- BOKO HARAM YASHAMBULIA KASKAZINI MWA NIGERIA.
- NAMNA BORA NA ASILIA YA KUTUNZA NGOZI
- NAMNA BORA YA KUTUNZA KUCHA NA KUEPUKA MARADHI SHA...
- HISTORIA NA MADHARA YA LIPSTICK KWA WANAWAKE
- ACT WAZALENDO YAMTUMBUA ANNA MGHWIRA
- KUNDI LA ISLAMIC STATE LASEMA LILIHUSIKA KWENYE SH...
- WACHAFUZI WA MAZINGIRA WATADHARISHWA.
- MUGABE AANZA KAMPENI ZA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2018
-
▼
June
(100)
No comments:
Post a Comment