Latest News

MAKAMU WA RAISI SAMIA SULUHU AWATAKA WAWEKEZAJI WA MAFUTA NA GESI KUNUNUA BIDHAA ZA HAPA NCHINI.

MAKAMU wa Rais Samia Suluhu Hassan amezitaka kampuni zilizowekeza katika sekta ya mafuta na gesi nchini kuhakikisha zinanunua huduma na bidhaa zinazopatikana nchini.
Mh. Samia Suluhu Hassani:Makamu wa raisi wa Jamuhuri ya muungano ya Tanzania.

Amesema hitaji la watoa huduma wa Kitanzania kunufaika linaendana na sheria ya mafuta ya mwaka 2015 inayosisitiza katika ununuzi wa bidhaa na huduma zinazopatikana ndani.
Samia ameyasema hayo wakati akizundua Jumuiya ya Watoa Huduma Katika Sekta ya Mafuta na Gesi Tanzania (ATOGS) jijini Dar es Salaam ambapo pia alipongeza uanzishwaji wa jumuiya hiyo kwa kuwa una lengo sawa na Serikali ya Awamu ya Tano.
“Na pale ambapo huduma na bidhaa hazipatikani nchini, basi makampuni hayo yanapaswa kununua kutoka kwenye makampuni ya ndani yenye wabia nje ya nchi,” amesema Samia.
Alifafanua kuwa sheria hiyo imezingatia maslahi ya wananchi ikitaka hisa za makampuni ya ndani kutopungua asilimia 25 na kwamba kwa kununua bidhaa na huduma kutoka ndani ya nchi, Watanzania wengi walioko vijijini watanufaika.

No comments:

Post a Comment

NAKUJUZA Designed by Templateism.com Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.
Published By Gooyaabi Templates