Latest News

EVERTON MBIONI KUMNYAKUA MNIGERIA HENRY ONYEKURU.

Everton wanakaribia kumnunua mshambuliaji chipukizi wa Nigeria anayevuma sana Henry Onyekuru kutoka klabu ya KAS Eupen ya Ubelgiji.
Henry Onyekuru.

Wanatarajwia kumnunua mchezaji huyo kwa £7m. Onyekuru, 20, alifunga mabao 22 katika klabu hiyo inayocheza ligi kuu ya Ubelgiji msimu uliopita.
Alikuwa amehusishwa na kuhamia Arsenal, West Ham United na klabu nyingine kadha Ulaya zilikuwa pia zinamtaka. Hata hivyo, mchezaji huyo, inaarifiwa tayari alifanyiwa uchunguzi wa kimatibabu Everton siku ya Jumatatu.
Anachukuliwa na mkurugenzi wa soka wa Everton Steve Walsh pamoja na meneja Ronald Koeman kuwa mchezaji atakayewafaa sana siku za usoni.
Onyekuru alichezea timu ya taifa ya Nigeria mara yake ya kwanza katika mechi ya kirafiki dhidi ya Togo mapema mwezi huu ambayo walishinda 3-0.

No comments:

Post a Comment

NAKUJUZA Designed by Templateism.com Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.
Published By Gooyaabi Templates