Latest News

WAFUNGWA WENGINE 930 WATOROKA GEREZANI NCHINI KONGO KINSHASA.

Gavana wa jimbo la Kivu ya Kaskazini Julien Paluku amesema zaidi ya wafungwa 930 wametoroka baada ya kutokea shambulizi na kuvunja gereza moja huko Congo DRC.
Hii ni takribani mara ya tatu kwa wafungwa kutoroka gerezani nchini Kongo

Watu 11 wameuawa katika tukio hilo Kaskazini Mashariki mwa mji wa Beni.
Haijajulikana ni nani haswa aliyefanya shambulizi hilo.
Siku ya Jumamosi wafungwa kadhaa walitoroshwa na mtu mmoja aliyekuwa na silaha.
Mwezi uliopita mamia ya wafungwa walitoroka katika jela moja kubwa mjini Kinshasa baada ya mtu mmoja aliyekuwa na silaha kuvamia jela hiyo usiku wa manane.

No comments:

Post a Comment

NAKUJUZA Designed by Templateism.com Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.
Published By Gooyaabi Templates