Mkuu wa wilaya ya Sengerema, Emanuel Kipole amewataka mawakala wazao la pamba wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza kutumia mizani sahihi kupima zao la Pamba ili kuepuka kumuibia mkulima.
Kauli hiyo aliitoa wakati alipokuwa kwenye semina ya mawakala wa pamba inayoshirikisha Wilaya tatu ambazo ni Sengerema, Nyang’hwale na Geita kutoka kampuni moja ya ICK iliyoingia mkataba na serikali kununua zao la pamba katika wilaya hizo.
Hata hivyo, Kipole alitoa wito kwa kampuni hiyo kuhakikisha inazingatia bei elekezi iliyotolewa na serikali msimu huu.
Nae Mkuu wa kituo cha Polisi wilaya ya Sengerema, Maili makori alitoa angalizo kwa wakulima ambao wameingia mkataba na kampuni hiyo kuhakikisha wanazingatia makubaliano waliojiwekea.
Kwa upande wao mawakala waliohudhuria semina hiyo wamemuhakikishia mkuu wa wilaya hiyo kwamba, watakuwa waadilifu kwa kusimamia sheria za ununuzi wa zao la pamba na si vinginevyo.
Na Veronica Martin
No comments:
Post a Comment