Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na watoto, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi Kigwangalla ameshiriki futari maalum iliyoandaliwa na Benki ya Biashara Afrika Tawi la Tanzania (CBA Tanzania) iliyokuwa maalum kwa ajili ya wadau na wateja wa benki hiyo, tukio lililofanyika katika Hotel ya Hyatty Regency, Kilimanjaro ijini Dar es Salaam jioni ya Juni 16.2017.
Dkt. Hamisi Kigwangalla ambaye alikuwa mgeni rasmi katika tukio hilo, aliimiza ushirikiano, Umoja na upendo kwa watanzania wote hasa katika kipindi hiki cha mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
DOKTA Khamisi Kigwangala. Naibu waziri wa Afya maendeleo ya jamii jinsia na watoto. |
Kwa upande wao CBA Tanzania walibainisha kuwa, tukio hilo ni sehemu ya kuboresha uhusiano na wateja na wadau wao. Mkurugenzi Mkuu wa benki hiyo Dk.Gift Shoko alisema: “Tunampongeza Naibu Waziri Dk. Kigwangalla kwa kufika na kujumuika nasi katika tukio hili maalum la Iftar. Pia tunawashukuru sana wateja wetu nchini kote kwa kuendelea kuiamini benki yetu katika kupata bidhaa na huduma za kibenki na ndio maana tunashirikiana nao sana katika maeneo maalum ambayo yanatukutanisha ili pia tuweze kujadiliana na kuboresha ushirika wetu kama tunavyokutana leo kwenye futari hii”. Alisema Dk. Shoko.
Dk. Shoko aliahidi kuwa Benki itaendelea kuboresha bidhaa na huduma zake ili ziendelee kuwa na ubora wa hali ya juu kabisa ikiwa ni pamoja na kubuni huduma mbalimbali za kuwarahishia maisha wateja wanapohitaji kupata huduma za kibenki na kuboresha shughuli zao.“Benki ya CBA Tanzania tunawatakia mfungo mwema wa Ramadhani lakini pia maandalizi mema ya sikukuu hapo baadae!,” alieleza.
CBA Tanzania ni sehemu ya CBA Group iliyopo katika nchi za Kenya, Uganda na Tanzania, CBA Tanzania ina matawi kumi na moja yaliyosambaa sehemu mbalimbali nchini.
No comments:
Post a Comment