Serikali imejidhatiti kutokomeza magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele ili kutimiza malengo ya kujenga uchumi wa viwanda na afya bora mpaka kufikia 2020.
Hayo yamesemwa na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohammed Kambi wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa mwaka unaolenga kupitia shughuli za mpango wa Taifa wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele.
Prof. Mohammed Kambi. Mganga mkuu wa serikali. |
“Tunataka mpaka kufikia 2020 tuwe tumetokomeza magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kama mabusha na matende ili kuweza kuinusuru nchi katika aina hii ya magonjwa yanayojitokeza katika nchi zinazoendelea hususan Tanzania” alisema Prof. Kambi.
Aidha Prof. Kambi amesema kuwa licha ya kudhibiti mabusha na matende pia wamejidhatiti kuzuia ugonjwa wa usubi na kichocho kabla ya kufikia 2025 ili kuendana na mpango wa dunia wa kudhibiti magonjwa hayo.
Kwa upande wake Mratibu wa Mpango wa Taifa Wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Dkt. Upendo Mwingira amesema kuwa wananchi wanatakiwa wajitokeze kupata dawa na tiba za magonjwa hayo kwan hazina madhara kwa binadamu.
Mkutano huo uliokutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya afya kutoka duniani kote umelenga kupata mpango kazi wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kwa mwaka 2017 na 2018 ili kuweza kupata njia za kudhibiti magonjwa hayo kama vile mabusha na matende, kichocho na usubi.
Na WAMJW Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment