Klabu ya Simba SC imeendelea kuimarisha kikosi chake baada ya kusajili wachezaji wawili, ambapokwa sasa imemsajili golikipa wa Azam FC, Aishi Manula kwa mkataba wa miaka miwili.
Aidha, meripotiwa kuwa Simba SC imemsajili Manula kwa kitita cha milioni 50 na atakuwa akilipwa milioni tatu kwa mwezi.
Aidha kwa upande wa uongozi wa Simba haujawa tayari kuzungumza kuhusu usajili huo na kuwa utatoa taarifa itakapokuwa tayari kufanya hivyo na itatoa taarifa kupitia app yake ya Simba app.
“Sisi Simba tuna utaratibu wetu wa kufanya usajili na kwa sasa hatuwezi kuzungumza jambo lolote, muda ukiwadia tutaoa taarifa na watu watajua ni nini kinafanyika,” amesema Makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange Kaburu wakati akifanya mahojiano na kituo cha redio cha E fm
No comments:
Post a Comment