Hospitali teule ya Wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza inakabiliwa na upungufu wa damu kwa kiasi kikubwa.
Kauli hiyo imetolewa na Mtalaamu wa Maabara Wilayani Sengerema, Alex Lweyemamu ikiwa leo ni siku ya uchangiaji damu salama duniani ambapo amewaomba wananchi kujitokeza na kujitolea kuchangia damu ili kuwasaidia watu wenye uhitaji wa damu.
Uhaba wa damu kwenye mahospitai unatokana na muitikio hafifu wananchi katika kuchangia damu. |
Lweyemamu amesema kuwa kwa wastani kwa mwezi mmoja hospitali hiyo inatakiwa ipate chupa za damu salama 350 lakini inashindwa kufikia kiwango hicho kutokana na mwitikio hafifu wa wananchi kujitolea damu kwani tangu kampeni ya uchangiaji damu ianze Juni mosi mwaka huu hadi June 14 ni jumla ya chupa 89 pekee zimechangiwa.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi waliowahi kuchangia damu salama wameitaka jamii kuwa na mwamuko wa kusaidia watu wenye uhitaji wa damu huku wengine wakiiomba serikali kutoa elimu juu ya umhimu wa uchangiaji damu.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Misheni Wilaya ya Sengerema, Devis Lusobangija ameiomba jamii kujitokeza kuchangia damu ili kuwaokoa watu wanaokabiliwa na upungufu wa damu.
Licha ya serikali, asasi za kiraia na viongozi wa dini kuhamasisha jamii ichangiae damu lakini mwitikio bado ni hafifu mpaka sasa.
Na Emmanuel Twimanye, Sengerema
No comments:
Post a Comment