Latest News

MOTO WAATHIRI HUDUMA YA NISHATI YA UMEME, NKASI MKOANI RUKWA

Watu wasiojulikana wamechoma msitu wa Kirando wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa ambao umeunguza miundombinu ya umeme ya Shirika la umeme Nchini TANESCO.
 
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jioni hii Juni 24, 2017 na Kaimu Meneja Uhusinao wa TANESCO makao Makuu, Bi. Leila Muhaji, imesema, uharibifu huo mkubwa wa miundombinu umeathiri upatikanaji wa umeme kwa wateja wa maeneo ya Kirando na Kipili wanaopata huduma ya umeme ya njia ya msongo mkubwa wa umeme unaopita kwenye maeneo hayo.
“Mafundi wa TANESCO waliofika kwenye eneo hilo, wameshuhudia uharibifu mkubwa ambapo miundombinu ya umeme imeungua na kusababisha hasara kubwa.” alisema Bi Leila katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.
 Leila amesema TANESCO inawaomba wananchi wote waishio kwenye maeneo hayo kutoa taarifa kwenye ofisi za TANESCO au kituo cha polisi kilicho karibu ili kuokoa miundombinu ya umeme kwa manufaa ya taifa.  
Amesema, tayari vyombo vya ulinzi na usalama kwa kushirikiana na TANESCO wameanza msako ili kuwabaini wahusika ili sheria ichukue mondo wake.
Na mwandishi wa K-VIS Blog 

No comments:

Post a Comment

NAKUJUZA Designed by Templateism.com Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.
Published By Gooyaabi Templates