Latest News

MAREKANI YAZIHAKIKISHIA USALAMA NCHI WANACHAMA WA NATO.

Rais wa Marekani Donald Trump ametoa ahadi maalum ya kujitolea kwake katika kufanikisha mkataba wa mataifa ya kujihami ya NATO, ambapo mataifa wanachama huwa yamekubaliana kulinda kila mmoja.
Kuliibuka wasiwasi miongoni mwa mataifa wanachama baada ya rais Trump kukosa kuunga mkono hadharani kipengee cha tano cha mkataba wa N
ATO, wakati alipozuru makao makuu ya NATO mwezi mei mjini Brussels
Makao makuu ya NATO
Makao makuu ya NATO mjini Brussels
Katika mkutano huo rais Trump alitaka mataifa wanachama kulipa pesa zaidi za kuimarisha ulinzi wa muungano huo.
Hata hivyo hapo jana baada ya mkutano na rais wa Romania , Klaus Iohannis, bwana Trump alisema, nikimnukuu "kwa hakika tuko hapa kulinda".

No comments:

Post a Comment

NAKUJUZA Designed by Templateism.com Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.
Published By Gooyaabi Templates