Latest News

TRUMP ABANWA TENA NA MAHAKAMA.

Mahakama ya rufaa nchini Marekani imemua kuwa uamuzi wa kuzuia mpango uliofanyiwa marekebisho wa marufuku ya rais Donald Trump kuzuia watu kutoka nchi sita za kiislamu utaendelea kuwepo. Majaji wamesema kuwa amri hiyo inakiuka sheria zilizopo za uhamiaji.


Rufaa hiyo iliyowasilishwa katika mahakama ya rufaa ya San Fransisco, ni kufuatia uamuzi uliotolewa kupinga raia wengi wao wakiwa kutoka nchi za Kiislam kuingia Marekani.
Hata hivyo mahakama haikusema kuwa serikali inatakiwa kuzipitia upya taratibu za ukaguzi kwa watu wanaoingia nchini humo.
Msemaji wa Ikulu ya Marekani Sean Spicer ameutetea msimamo huo wa rais Trump, akisema amri hiyo ilitolewa kwa ajili ya ulinzi wa Marekani.

No comments:

Post a Comment

NAKUJUZA Designed by Templateism.com Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.
Published By Gooyaabi Templates