Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Mwanza inamshikilia James Edward ambaye ni Afisa Mtendaji wa Kata ya Kishiri wilayani Nyamagani Jijini Mwanza kwa kosa la kupokea rushwa kiasi ya shilingi laki mbili.
Akizungumza na vyombo vya habari ofisini kwake mkuu wa Takukuru mkoani Mwanza Ernest Makale amesema kuwa mtuhumiwa amekamatwa baada ya mtu aliyeomba fedha hizo kutoa taarifa kwa taasisi hiyo kisha taasisi hiyo kuandaa mtego uliofanikisha kumkamata afisa mtendaji huyo.
Makale amesema kuwa Mtendaji huyo alijifanya kuwa ni mhandisi wa halmshauri ya jiji la Mwanza na kujitambulisha kwa mfanyabiashara mmoja aitwae Alex anaefanya biashara zake kando ya hifadhi ya barabara Mkolani jijini humo ambapo amemuomba kiasi cha shilingi milioni 1 ili asimuondoe katika eneo hilo.
Aidha amesema kuwa walipoendelea na uchunguzi kwa mtuhumiwa huyo amebainika kuwa na makosa mengine yakiwemo ya kuwa na fedha ambayo haijulikani ameitoa wapi pamoja na kuwa na mashaka na elimu yake
Kwa upande wake mtuhumiwa wa tukio hilo ambae ni Afisa Mtendaji wa mtaa wa Mtakuja, James Edward akungumzia tukio hilo amekana kutenda kosa hilo.
Na Veronica Martine
nzuri
ReplyDelete