Waziri mkuu mstaafu na mwanachama wa Chama cha Chadema Mh: Edward Lowassa, amehojiwa na kuondoka katika ofisi ya mkurugenzi wa uchunguzi wa jinai baada ya kutakiwa kufika katika afisi hiyo siku ya Jumatatu kwa sababu zisizojulikana .
Edward Lowasa: Waziri mkuu mstaafu wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania. |
Kulingana na gazeti la The Citizen, Bwana Lowassa ambaye alitakiwa kuwasili katika afisi ya DCIO muda wa saa nne aliwasili saa tatu na dakika 58 asubuhi.
Msafara wake ulikuwa na magari sita ikiwemo magari mawaili ya polisi yaliokuwa na polisi waliojihami .
The Citizen linasema kuwa usalama ulikuwa umeimarishwa katika barabara ya Ohio.
Waandishi habari walikatazwa kuchukua picha za bwana Lowassa.
Katika mahojiano ya simu na gazeti la The Citizen, alisema kuwa anashuku kwamba agizo hilo la kutakiwa kujiwasilisha linatokana na matamshi aliyotoa mjini Dar es salaam siku ya Ijumaa wakati wa hotuba ya Iftar.
Wakati wa hotuba hiyo, alimtaka rais Magufuli kuwaachilia huru wahubiri wa Kiislamu ambao walikuwa wamekamatwa kwa zaidi ya miaka minne bila kesi zao kuamuliwa.
No comments:
Post a Comment