Baadhi ya mataifa ambayo yana rikodi mbaya zaidi ya uchafuzi wa mazingira ya bahari kutokana na plastiki wamehaidi kuanza kuchua hatua ya kufanyia usafi maeneo yao ya bahari .
Wawakilishi kutoka nchi za China,Ufilipino,Indonesia na Thailand katika kongamano la umoja wa mataifa linaloangazia hali ya bahari duniani wamesema watafanya juhudi kubwa kuondoa taka za plastiki kwenye bahari.
Utafiti wa hivi karibuni umethibitisha kuwa taka za plastiki zinaathari pia viumbe wa baharini.
Plastiki nyingi zinatoka katika mikondo ya mito mikuuu 10 huko barani Asia.
Mchambuzi wa BBC wa masuala ya mazingira anasema ni vigumu kusema kwamba ahadi hizo zinaweza kuweka kwenye sheria ya kukabiliana na tatizo hilo.
NA:BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment