Latest News

MANCHESTER UNITED WAANZA NA MLINZI WA BENIFICA

Manchester United wameafikia makubaliano ya kumsaini mlinzi raia wa Sweden Victor Lindelof kutoka Benfica kwa kima cha pauni milioni 31.
Victor Lindelof
United wanasema kuwa kilichobakia ni makubaliano ya kibinafsi na uchunguzi wa kiafya ambavyo viitafanyika wiki ijayo.
Lindelof, ambaye ameichezea nchi yake mara 12 anatarajiwa kushiriki mechi ya kirafiki nchini Norway siku ya Jumanne.
Mchezaji huyo mwenye maiak 22 ambaye amekuwa akiichezea Benfica tangu mwaka 2012 atakuwa mchezaji wa kwanza kusainiwa na Man U msimu huu.
Lindelof alicheza mara 47 klabu hiyo ya Ureno msimu uliopita.

No comments:

Post a Comment

NAKUJUZA Designed by Templateism.com Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.
Published By Gooyaabi Templates