Latest News

UFINYU WA MVUA NA HALI YA KUONGEZEKA KWA JOTO VYA BADILISHA RANGI YA ZIWA.

Ziwa moja la maji ya chumvi mjini Melbourne Australia limegeuka na kuwa na rangi ya waridi kutokana na mwanga wa jua, joto na mvua chache.
Maafisa wa mbuga za wanyama pori wamesema kuwa mwani unaomea katika ziwa hilo chini ya bustani ya Westgate hutoa rangi nyekundu.
Maji ya Ziwa yakiwa yamebadilika rangi na kuwa na muonekano wa rangi nyekundu.

Furahia mandhari lakini nawashauri kutoshika maji hayo,alisema victoria.
Hali hiyo pia hutokea katika eneo la salina Torrevieja katika ziwa la Dusty Rose na ziwa la Retba nchini Senegal.
Mwanasayansi wa maswala ya kuhifadhi katika bustani ya Victoria amesema kuwa rangi hiyo imesababishwa na mwani kwa jina Dunalliela.
''Sisi hupata maoni kwamba bustani hiyo huonekana kana kwamba ni kiwanda cha rangi kilichomwaga rangi hiyo kwa bahati mbaya''.
Dkt Norman amesema kuwa ijapokuwa maji hayo sio hatari ,hangemruhusu mtu kuogelea.
Wasimamizi wa ziwa hilo wamesema kuwa wanataraji kwamba ziwa hilo litabadilika na kuwa yangu yake ya kawaida wakati joto litakapokwisha na mvua kuongezeka.
NA:BBC SWAHILI

No comments:

Post a Comment

NAKUJUZA Designed by Templateism.com Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.
Published By Gooyaabi Templates