Askari jeshi mmoja afariki katika shambulizi lililotekelezwa Qatif nchini Saudi Arabia.
Askari mmoja afariki na wengine wawili kujeruhiwa katika shambulizi lililotekelezwa dhidi yao wakiwa katika kazi yao Qatif.
Taarifa hiyo ilitolewa mapema Jumatatu na waziri wa mambo ya ndani wa Saudia Arabia.
Tukio hilo limetokea Mashariki mwa Saudia Arabia.
Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani Mansur al Turki alisema kuwa shambulizi hilo lililotekelezwa Jumapili usiku Mansura ni shambulizi la kigaidi.
No comments:
Post a Comment