Latest News

UCHAGUZI MKUU KONGO KINSHASA BADO KITENDAWILI

KANISA KATOLIKI LA TISHIA KUJITOA KWENYE MAZUNGUMZO YA UPATANISHI WA AMANI YANAYOENDELEA NCHINI JAMUHURI YA DEMORASIA YA KONGO


Ghasia zimetokea kwenye baadhi ya maeneo nje kidogo ya mji mkuu wa Jamhuri ya demokrasia ya Kongo Jumanne baada ya Kanisa katoliki kujitoa katika nafasi yao ya usuluhishi.
Maaskofu hao walikuwa wanafanya juhudi za kuzikutanisha pande mbili zenye mgogoro yaani serika na upinzani katika mazungumzo yaliyokuwa yamekusudia kutafuta ufumbuzi wa kucheleweshwa kwa uchaguzi mkuu wa uraisi mwaka huu.
Waandamanaji walionekana wakichoma matairi ya magari katika makutano ya barabara ambapo waliandamana katiaka njia kadhaa huko Kinshasa jambo lililopelekea maduka mengi mjini hapo kufungwa na baadhi ya shule kuwataka wazazi waje kuwachukua watoto wao.
Kipindi cha utawala cha raisi Joseph Kabila kilifikia kikomo mnamo mwezi Disemba mwaka jana lakini uchaguzi ulikuwa haujafanyika katika kile serikali ya Kongo ilidai kuwa ni matatizo ama ufinyu wa bajeti katika nchi hiyo na kupelekea kuzuka kwa maandamano yenye fujo ambayo yalisababisha vifo vya watu takribani 40.
Maaskofu wa kanisa Katoliki walijiondoa katika usuluhishi wa mgogoro huo Jumanne ya wiki hii baada ya utekelezaji wa makubaliano hayo kukwama na kuwepo kwa uwezekano wa kuzuka upya kwa uvunjifu wa amani katika taifa hilo ambalo limekumbwa na mfululizo wa mapigano ya kuwania madaraka

No comments:

Post a Comment

NAKUJUZA Designed by Templateism.com Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.
Published By Gooyaabi Templates